Friday, March 12, 2010











Moja ya kazi nilizofanya, Akiba Advert

Thursday, March 11, 2010


Tunadesign Matangazo na mambo yote yanayohusu graphics mbalimbali kama unavyoona

Monday, February 1, 2010




Lucinda Dickey aka Kelly ni mmoja wa washiriki wa sinema ya muziki wa BreakDance ambayo ilitamba sana miaka ya 1984 akiwa na wenzake
kama Michael Chambers aka Electric Boogaloo pamoja na Adolfo Quinones aka Shaba-doo. Pia ameshiriki kwenye baadhi ya Sinema kama Ninja III: The Domination (1984)Cheerleader Camp (1988), The Case of the Defiant Daughter (1990) , Breakin' 2: Electric Boogaloo (1984). Lucinda hivi sasa anaishi California na mumewe anayeitwa, Craig Pilligian ambaye ni mtayarisha mkuu wa kipindi maarufu cha TV kinachoitwa "Survivor" pamoja na watoto wao wawili.

Angalia picha mbalimbali za Lucinda za zamani na hivi sasa.

Jamaa bado yupo kwenye fani yake kama kawaida. Kama unamkumbuka kwenye Komedi alizocheza  za "Family Matters" na ndizo zilizompatia umaarufu mkubwa. Huyu jamaa ni nani?  tumcheki kiundani kidogo!


Jamaa anaitwa "Jaleel Hahmad White" ndilo jina lake la kuzaliwa, pia anajulikana kwa jina Steve, kwenye Komedi alizowahi kuigiza kama "Family Matters".  Alizaliwa tarehe 27 Novemba 1976, huko Pasadena, California, USA. Aligraduate katika Chuo cha "UCLA Film School" mwaka 2001.

Pia alisoma katika shule ya  "Henry E. Huntington Middle School" huko San Marino, California.

Katika maisha yake ya utotoni alipendelea kutengeneza ice cream akiwa nyumbani kwao. Pia alikuwa akipendelea kuandika hadithi fupifupi pamoja na kuchora katuni mbalimbali.



Baba yake alikuwa anaitwa Michael, ni daktari wa meno, wakati mama yake ni Gail, ni mama wa nyumbani.

Kwa mara ya kwanza alipofanya video yake ya kwanza kama Steve Urkel, vijana kama hamsini waliokuwa wakimuangalia wakati wa kufanya shooting walimshangilia na kuanza kumwita jina la  "Urkel! Urkel! Urkel!" na baada ya hapo mtayarishaji wake alianza kugundua kama kijana alikuwa na kipaji alichojaliwa na mungu.



Alikuwa akishilia  namba 37 kwenye orodha ya  "VH1" kati ya watoto 100 mastaa waliokuwa kwenye chati za juu kwa kipindi hicho.

Alipendekezwa kuwa muigizaji mkuu wakati wa kuigiza Komedi ya  "Saved by the Bell" mwaka 1989

Baadhi ya Komedi na Sinema alizowahi kushikiri ni pamoja na  

"Family Matters"  ambapo alicheza kwenye vipande  kama  - A Pirate's Life for Me,Busted , Life of the Party, High Hopes, Cousin Urkel,  pia alicheza sinema za Dreamgirls, Who Made the Potatoe Salad? na nyingine nyingi. Huyo ndiye Jaleel Ahmad White aka Steve



.



Waasisi wa Bongo Hip Hop NiggaOne kulia na D-Robby kushoto enzi za uhai wao kama wanavyoonekana, huwezi kuongelea bongo fleva ilivyoanza bila kuwataja hawa jamaa. Stori zaidi kuhusu jamaa walivyoitambulisha bongo fleva hapa nchini inakuja hivi karibuni, tega mingo!